0754 909 397 info@sttheresia.go.tz Open 24 Hours Emergency: 0612 898 599

ST. THERESA HOSPITALI WENDA, IRINGA

Wenda, Iringa - Tanzania

KUHUSU ST. THERESA HEALTH CENTER – WENDA

KUHUSU ST. THERESA HEALTH CENTER – WENDA
Huduma kwa Upendo Afya na ustawi wa jamii

Kuhusu Kituo cha Afya St. Theresa – Wenda

ST. THERESA HEALTH CENTRE – WENDA KUHUSU KITUO CHA AFYA Kituo hiki cha afya kinamilikiwa na Shirika la Masista Wamisionari wa Mt. Theresa wa Mtoto Yesu la Jimbo Katoliki la Iringa. Kituo hiki kilianzishwa kufuatia ombi la wakazi wa Kijiji cha Wenda ambao walihitaji kuwepo kwa huduma za afya katika eneo lao, kwa kuwa wananchi hao walikuwa wakipata changamoto kubwa katika kupata huduma za afya. Kwa hiyo, kwa umoja wao waliomba msaada kwa Masista wa Shirika la Mt. Theresa wa Mtoto Yesu ili waje na kuanzisha huduma hiyo. Baada ya Masista hao kukubali ombi hilo, kiongozi wa kijiji, Gaudensio Malangalila, pamoja na familia yake, walitoa eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 26,668, sawa na ekari 7. Tunawashukuru kwa ukarimu wao. Kituo hiki kilianza kutoa huduma mwaka 1998 kama zahanati, kikitumia nyumba ya kiongozi wa kijiji Gaudensio Malangalila. Kituo kilisajiliwa rasmi na Wizara ya Afya, Wazee na Ustawi wa Jamii tarehe 31 Julai 2008 kama kituo cha afya, kikiwa na namba ya usajili 111231. Kituo hiki kinahudumia zaidi wakazi wa Kata ya Mseke, ambao shughuli yao kuu ni kilimo. Kituo kina jumla ya vitanda 43 na hutoa huduma za wagonjwa wa nje kwa wastani wa wagonjwa 17,800 na huduma za wagonjwa wa kulazwa kwa wagonjwa 1,946 kwa mwaka. Aidha, kutokana na kuwepo kwa madaktari bingwa na huduma za vipimo vya maabara, kituo hiki hupokea wagonjwa kutoka nje ya wilaya, kama vile Mufindi, Manispaa ya Iringa na Kilolo, pamoja na kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Morogoro, Dodoma, Mbeya, Njombe, Tanga na Dar es Salaam.

Dira, Dhima na Ahadi Yetu

DIRA YETU

Dira

Kuwa hospitali inayoongoza katika ngazi ya wilaya katika kutoa huduma za afya zenye ubora wa hali ya juu kwa wote.

DHIMA YETU

Dhima

Kutoa huduma za afya zinazomlenga mgonjwa, zinazopatikana kwa urahisi, zenye gharama nafuu na zinazokidhi mahitaji ya jamii tunayohudumia kwa upendo na huruma.

AHADI YETU

Ahadi

Tumejizatiti kwa dhati kutoa huduma bora za kitabibu, kulinda utu wa wagonjwa na kudumisha viwango vya juu vya maadili katika utoaji wa huduma za afya. Tukiongozwa na imani yetu na kujitolea kwa jamii, tunaahidi kuendelea kuboresha huduma zetu ili kila mtu anayefika katika kituo chetu apate matibabu kwa wakati, kwa heshima na kwa ubora wa hali ya juu, bila kujali historia au hali yake.

Maadili Yetu ya Msingi

Maadili yanayotuelekeza katika kutoa huduma bora za afya kwa jamii.

01

Huruma

Kumhudumia kila mgonjwa kwa upendo, uelewa na wema wa dhati

02

Utu na Heshima

Kuheshimu haki za binadamu na thamani ya kila mtu

03

Uadilifu

Kudumisha uwazi, uaminifu na viwango vya juu vya maadili

04

Ubora

Kutoa huduma bora za afya kupitia kujifunza na kuboresha huduma kila wakati

05

Uaminifu wa Imani

Kuheshimu utambulisho wetu wa Kikatoliki na kujitolea kwa ajili ya jamii

06

Ujumuishi

Kutoa huduma kwa kila mtu bila kujali historia au hali yake

Huduma za Afya Zinazotolewa

Kituo cha Afya St. Theresa – Wenda kinatoa huduma mbalimbali za afya kwa wagonjwa na jamii.

1
Huduma za Wagonjwa wa Nje (OPD)
2
Huduma za Wagonjwa wa Kulazwa (IPD)
3
Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto (RCH)
4
Kliniki ya Huduma na Tiba (CTC)
5
Huduma za Maabara
6
Huduma za Macho
7
Huduma za Afya ya Kinywa na Meno
8
Kliniki Maalum ya Tiba ya Ndani
9
Huduma za Tiba ya Mazoezi na Urekebishaji wa Mwili (Physiotherapy and Rehabilitation)
10
Huduma za Upasuaji
11
Huduma za Radiolojia (X-Ray/Vipimo vya Picha)

Huduma Zinapatikana Saa 24 kwa Siku

Kituo cha Afya St. Theresa hufanya kazi saa 24 kwa siku, siku 7 za wiki (24/7). Ratiba ya kila siku huanza saa 1:30 asubuhi kwa ibada fupi ya asubuhi (sala) inayodumu kwa dakika 20. Baada ya hapo hufanyika kikao cha taarifa za asubuhi ambapo wahudumu wa zamu ya usiku hukabidhi taarifa za wagonjwa kwa wahudumu wa zamu ya asubuhi. Huduma za dharura zinaendelea kutolewa wakati huu, huku huduma nyingine za kawaida za afya zikianza saa 2:00 asubuhi. Huduma za daktari bingwa wa Tiba ya Ndani zinapatikana kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 9:30 alasiri, kwa siku tatu kwa wiki: Jumatatu, Jumatano na Ijumaa.

Ratiba ya Kuwatembelea Wagonjwa Wodini

Muda wa Ziara Muda Asubuhi Saa 12:00 – 12:30 asubuhi Mchana Saa 6:00 – 6:30 mchana Jioni Saa 10:00 – 11:00 jioni